Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-
Sheikh Juma Shughuli, akizungumza kupitia Kituo cha Televisheni cha Mahdi TV jijini Nairobi, Kenya, amesisitiza kuwa imani inatakiwa kuendana na vitendo. Amesema kuwa haitoshi kuwa na wakati mmoja na Mtume Muhammad (s.a.w.w) au kuishi katika zama zake; jambo muhimu ni jinsi mtu anavyotenda.
Akaeleza kuwa mafundisho ya Mtume (s.a.w.w) yanapaswa kuongozwa na vitendo. Ikiwa matendo ya mtu yanaendana na maelekezo ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi imani yake inakuwa imetimizwa kwa vitendo vyema. Sheikh Shughuli aliongeza kuwa masahaba wa Mtume (s.a.w.w) wanatathminiwa kwa matendo yao, sio kwa usuhuba wao au kuishi pamoja na Mtume (saww).
Hii ni tafsiri muhimu inayoonyesha kuwa ushuhuda wa imani unaonyeshwa kivitendo, si kwa historia au usuhuba wa Mtu kwa Mtume au kuishi Zama moja na Mtume (saww).
Your Comment